Pages

KARIBU NASHERA HOTEL, MOROGORO - | Boma Road, LITI Area P.O. Box 237, Morogoro | Tel. +255 23 26139

Feed icon

Sunday, May 25, 2008

TUJADILI PAMOJA...

Ikiwa ni siku chache baada ya wasanii na filamu wanaowania/zinazowania tuzo za vinara kwa mwaka huu kutajwa, tayari kumeibuka malalamiko kuwa kuna upendeleo.

Malalamiko hayo yameshuka baada ya wasanii na wadau mbalimali wa filamu kudai kuwa kukosekana kwa mastaa wa muda mrefu katika tuzo hizo ni kama kuwakomoa au kuwaangusha kisanii.

Wasanii ambao wametajwa kuwa na uwezo mkubwa katika game na majina yao yamekosekana ni pamoja na Vincent Kigosi ‘Ray’, Steven Kanumba ‘Kanumba’, Ndumbangwe Misayo ‘Thea’, Mwanaidi Suka ‘Mainda’ Blandina Chagula ‘Johari’, Alen Raymond ‘Bishanga’, Tecla Mgaya ‘Aisha’, Bakari Makuka ‘Beka’, Ally Taua ‘Bonta’, Ivon Cherry ‘Monalisa’ na wengineo.

Hizi ni hisia na maoni mbalimbali ya wadau wa tasnia hiyo niliyoyanasa katika Blog mbalimbali za Kibongo. Baada ya kunasa minong’ono hiyo nikaona ingekuwa ni vyema kama wadau wengine wa hapa bomani wakatoa maoni yao.

Je, wewe unasemaje? Ni kweli haki haikutendeka au ni blablaa za wakosaji? Changia...

6 MAONI YAKO:

waukweli said...

Yap shaluwa mimi kama mimi waukweli sijajua ni vigezo gani wamechukua ili kuwapata hao vinara wetu tunzo mtu kama kanumba si wakukosa kabisa,mayb wanamaana yao,tutaona itakapofikifia mwisho.

Anonymous said...

no comments

Anonymous said...

Tuzo za siku hizi watu wameamka bwana, hawaangalii sura au kujulikana kwa mtu, kinachoangaliwa ni uwezo wa msanii husika katika sanaa. Sioni kama kuna uendeleo wowote katika mjucho huo wa awali. Haki itatendeka tu. Achana haya mastaa uchwara. Bi sana waamndaji, endeleeni hivyo hivyo. Tusubirni mwisho kwanza, uache lawama za kijinga. Mdau wa filamu, Dar

waukweli said...

Mdau wa Filam nchini au Duniani nikisema hivyo sijakosea,Ni vigezo gani vilivyochukuliwa nataka kujua hilo,na sina maana kuwa watu wanaangalia sura hapana ningesema sura wapo wengi wauza zura,Na mtu akiwa amefanya kazi kwa bidii hatuna budi kumsifia na kumpasurpot na kununua kazi yake, kwa nini tusiseme na hapo hapo sura ikawa inalipa why tusisema KWA NINIII???,kwa hilo tumechoka kuburuzwa,Nashukuru Shaluwa Umeliona hilo na umetuwekea hii mada ili tuseme ukweli,sisi wa Tanzania ebu tuchecki itakavyokuwa MWISHO WAKE ,Nawapa Hongera sana waandaaji wa Tunzo ya Filam Tanzania.Ila kazi kwenu.Habari ndio hiyo.

Anonymous said...

iwe ni wivu au vyovyote itakavyokuwa lakini hapo lazima kuna... kwanini wale mastaa ambao wote tunajua ni waanzilishi wanakosa katika hilo shindano lao? kwahiyo mzee kipara naye anauza sura? kuna msanii mzuri kama claudi, mbona haonekani katika hizo tuzo, acheni hizo bwana, mi nahisi kama mshindi tayari ashajulikana, wanatuzuga tu. wabongo bwana hawapendi kabisa kuendesha mambo kwa haki. sijui kama hapio kunahaki jamaninyie mwasemaje?

Anonymous said...

Huyo kanumba mnayesema ni msanii mzuli, wala mimi sioni uzuli wake zaidi ya kujigamba kwenye magazeti. anasema anatuzo kibao mbona sasa hizi za bongo zenyewe zinamshinda. hana ishu kazi kuiga wanaigeria tu hana rorote huyo.